Raia 20 wa kigeni wauawa Bangladesh

Watu 20 wote wakiwa raia wa kigeni
wameuawa wakati wa shambulio linalodaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa
Islamic State katika mgahawa mmoja nchini Bangladesh,kulingana na
maafisa.
Wapiganaji walivamia mgahawa wa Holey Artisan mjini Dhaka
jioni siku ya Ijumaa kabla ya vikosi vya usalama kuingia yapata saa 12
baadaye.Wapganaji sita waliuawa huku mmoja akikamatwa kulingana na msemaji wa serikali.

Kundi la Islamic State limekiri kutekeleza shambulio hilo.
Waathiriwa wengi walidaiwa kutoka Itali na Japan.
Brigedia wa jeshi nchini humo jenerali Asraf Chowdhury alisema kuwa waathiriwa walishambuliwa na silaha kali.
Raia 20 wa kigeni wauawa Bangladesh
Reviewed by Ino
on
3:23:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment