Obama atoa pole kwa Uturuki
Rais wa Marekani
Barack Obama amemwambia Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoÄŸan kuwa nchi
ya Marekani ipo pamoja na watu wa Uturuki katika wakati huu mgumu baada
ya kushambuliwa kwa uwanja wake wa ndege wa Istanbul kwa mabomu ya
kujitoa muhanga siku ya Jumanne.
Obama anasema kuwa amempigia simu Rais wa Uturuki kumpa salam za rambirambi sambamba na kusisitiza dhamira ya nchi yake kuendeleza mapigano dhidi ya IS.
Shambulio hilo linatajwa kuwa limeuwa watu wengi zaidi nchini humo ikilinganishwa na mashambulizi kadhaa yaliyopita.
Obama atoa pole kwa Uturuki
Reviewed by Ino
on
12:47:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment