NCHI 7 AFRIKA ZENYE UWEZO MKUBWA KIJESHI
7. LIBYA
Mapinduzi yaliyofanywa na Libya mwaka 2011yalishangaza kutokana na uwezo
wa jeshi la nchi hiyo ambayo ina watu takribani milioni 6.
Hata hivyo libya wana vifaru vya kivita (tanks) 500, Magari ya kurushia
mabomu ya makombora (rocke projectors) 800, magari ya silaha za
kupigania vita (armored fighting vehicles) 2500, magari ambayo yana
mkonga kama wa kifaru (Howitizer au Self propelled gun) 400, AT Weapons
(Anti-Tank Weapons) Silaha za kuangamiza vifaru 1050, Helikopta za
kivita 121, Ndege za kivita zaidi ya 600 pamoja na serikali hiyo kutoa
dola za kimarekani ($880 million) kwenye Wizara ya Ulinzi kila mwaka
katika nchi hiyo.
6. KENYA
Nchi ya Kenya ipo katika ukanda wa Afrika Mashariki na ina idadi ya watu takribani milioni 43.
Kenya ina idadi ya vifaru vya kivita 186, magari ambayo yana mkonga kama
wa kifaru (Howitizer au Self propelled gun) 30, Ndege za kivita 148,
Helikopta za kivita 48, Viwanja vya ndege kwa ajili ya kufanyia mazoezi
na ndege za kivita 194. Kenya hutoa $5 Billion katika Wizara ya Ulinzi
ya nchi hiyo kila mwaka.
5. ALGERIA
Nchi ya Algeria ina idadi ya watu zaidi ya milioni 35 na nchi ya 34 duniani kuwa na idadi kubwa ya watu.
Nchi ya Algeria ina vifaru vya kivita zaidi ya 1000, magari ya silaha za
kupigania vita (armored fighting vehicles) 1800, Ndege za kivita zaidi
ya 400, Helikopta za kivita 136, Nyambizi 3, Meli za kivita za maeneo ya
pwani ya bahari (Coastal Craft) 12. Serikali ya Algeria hutenga zaidi
ya $8 Bilioni kwa ajili ya Ulinzi katika nchi hiyo kila mwaka.
4. NIGERIA
Nchi ya Nigeria iansemekana ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu Afrika kwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 73.
Nchi ya Nigeria ina vifaru vya kivita 363, magari ya silaha za kupigania
vita (armored fighting vehicles) zaidi ya 1400, Ndege za kivita 294,
Helikopta za kivita 84, Viwanja vya ndege kwa ajili ya kufanyia mazoezi
na ndege za kivita 53, na ina watu ambao ni milioni 50 ambao wanafanya
kazi na hivyo imepelekea bajeti ya nchi hiyo kwenye ulinzi kila mwaka
kuwa $2.2 Bilioni.
3. AFRIKA YA KUSINI
Nchi hiyo ipo chini kusini kabisa mwa bara la Afrika. Nchi hiyo ina
idadi ya watu zaidi ya milioni 50n na nchi ya 24 duniani kuwa na watu
wengi.
Afrika ya kusini ina vifaru vya kivita 250, Magari ya kurushia mabomu
ya makombora (rocket projectors) 240, magari ya silaha za kupigania
vita (armored fighting vehicles) 1590, Manuwariza kivita 4, Ndege za
kivita 240, Nyambizi 3 pamoja na chi hiyo kutenga $5 milioni katika
masuala ya Ulinzi ya nchi hiyo kila mwaka.
2. ETHIOPIA
Ethiopia ina idadi ya watu milioni 84 na ni nchi ya kwanza Afrika kupata uhuru wake.
Nchi ya Ethiopia ina zaidi ya vifaru vya kivita 300, magari ya silaha
za kupigania vita (armored fighting vehicles) 1200, Ndege za kivita 147,
Helikopta 68 zinazoweza kuvafanyia uvamizi sehemu yoyote ile na
serikali ya Ethiopia inatenga $300 milioni kwa siku 365 kuimarisha
ulinzi nchini humo.
1. MISRI (EGYPT)
Nchi ya Misri ina idadi ya watu milioni 83.
NCHI 7 AFRIKA ZENYE UWEZO MKUBWA KIJESHI
Reviewed by Ino
on
10:18:00 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment