Viazi si salama kwa wanawake wajawazito

Utafiti wasema viazi vya kukaangwa vinachangia maradhi ya kisukari kwa wanawake wajawazito
Ulaji wa mara kwa
mara wa viazi, bila kujali kama ni vya kuchemshwa au vya kukaangwa ama
chips, unaweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kuwa katika hatari ya
kupata maradhi ya kisukari wakati wa ujauzito, wameeleza watafiti wa
Marekani.
Hii labda ni kwa sababu wanga uliomo katika viazi unaweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya sukari zaidi, wanasema.
Wanawake wajawazito watakiwa kupunguza ulaji wa viazi vya kukaangwa(chips) kuepuka ugonjwa wa kisukari
Utafiti wao ulihusisha wanawake wajawazito zaidi ya 21,000.Lakini watafiti wa Uingereza wanasema ushahidi huo una mapungufu na kuongeza kuwa watu wengi wanahitaji kula zaidi vya wanga ili kupata nyuzi nyuzi, pamoja na matunda na mboga
Utafiti huo wa BMJ unahusu ulaji wa viazi hadi kiwango cha kuwa na uwezekano wa hatari ya kuugua kisukari.

Ulaji wa mboga mboga nyingine unaweza kuzuia hatari ya kisukari
Wataalam wa masuala ya lishe nchini Uingereza wanasema vyakula vyenye wanga ama vya kuongeza nguvu na joto mwilini kama vile viazi, vinapaswa kuwa theluthi moja ya vyakula vinavyoliwa na watu.
Utafiti huo unatarajia kuchunguza nini chanzo cha maradhi ya kisukari yanayowapata baadhi ya wanawake wawapo wajawazito .
Utafiti huu umefuatia wauguzi wawili waliopata ujauzito kati ya mwaka 1991 na 2001. Hakuna hata mmoja wao aliyewahi kuwa na maradhi ya kudumu kabla ya ujauzito.
Source : BBC Swahili
Viazi si salama kwa wanawake wajawazito
Reviewed by Ino
on
7:10:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment