Valcke avuliwa madaraka Fifa

Kamati ya maadili ya Fifa imependekezwa Valcke apigwe marufuku miaka tisa
Katibu mkuu wa
Shirikisho la soka duniani Fifa aliyekuwa amesimamishwa kazi Jerome
Valcke ameondolewa rasmi kutoka kwenye wadhifa huo na shirikisho hilo.
Mfaransa
huyo, 55, kwa sasa amesimamishwa kujihusisha na shughuli zozote za
kandanda baada ya kudaiwa kuhusika katika njama ya kufaidi kutokana na
mauzo ya tiketi za Kombe la Dunia.Fifa imependekeza apigwe marufuku kuhusika katika shughuli zozote za soka kwa miaka tisa.
Valcke, ambaye pia anakabiliwa na tuhuma za ufisadi, amekanusha madai hayo.
Valcke avuliwa madaraka Fifa
Reviewed by Ino
on
7:12:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment