Jimenez akamatwa Guatemala
Marekani inafanya uchunguzi kuhusiana na ufisadi katika shirikisho la kandanda duniani FIFA.
Polisi nchini
Guatemala wamemkamata aliyekuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka
nchini humo kama sehemu ya uchunguzi unaoendeshwa na marekani kuhusiana
na ufisadi katika shirikisho la kandanda duniani FIFA.
Mshukiwa
huyo Brayan Jimenez, amekuwa mafichoni tangu mwezi uliopita wakati
Marekani ilipotoa idhini ya kukamatwa kwa maafisa 16, wa shirikisho la
soka, katika kanda ya America ya Kusini.Mshukiwa huyo alikamatwa na polisi katika makaazi ya kibinafsi, katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Wakili wake Francisco Garcia Gudiel, amesema sasa atafanya kila juhudi ili mshukiwa huyo asihamishwe hadi Marekani kufunguliwa mashtaka.

Platin na Blatter wote walituliwa kwa miaka minane kutokana na ufisadi katika FIFA
Jimenez alikuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Guatemala Tangu mwaka wa 2010 hadi 2015.
Waendesha mashtaka nchini Marekani wanasema kuwa Jimenez na aliyekuwa katibu mkuu wake jenerali Hector Trujillo, walilipwa hongo ya mamilioni ya madola, ili kuuza haki za utangazaji za mechi za kufuzu za kombe la dunia la mwaka wa 2018.
Trujillo alikamatwa mwezi uliopita nchini Marekani. Kufikia sasa Marekani imewafungulia mashtaka watu 40 kama sehemu ya uchunguzi wake kwenye kashfa ya ufisadi inayokumba FIFA.
Source: BBC Swahili...
Jimenez akamatwa Guatemala
Reviewed by Ino
on
7:05:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment