Samatta azawadiwa na serikali ya Tanzania

Samatta aliibuka mfungaji mabao bora ligi ya klabu bingwa Afrika 2015
Mchezaji bora wa
Afrika kwa wachezaji wa nyumbani Mbwana Samatta amekabidhiwa sehemu ya
ardhi na serikali ya Tanzania kufuatia uhodari wake uliomwezesha
kuondoka na tuzo hiyo na kuisaidia TP Mazembe kutwaa kombe la vilabu
bingwa Afrika.
Mchezaji huyo pia alitunukiwa zawadi nyinginezo
kwenye hafla iliyoandaliwa ili kusherekea mafanikio yake katika soka
yaliyoiweka Tanzania katika ramani ya soka.Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wadau wa michezo nchini Tazania wakiwemo waziri wa michezo Nape Nnauye na Thomas Ulimwengu ambaye ni mchezaji mwenza wa Samatta.
Amepewa kipande cha ardhi eneo la Kigamboni, Dar es Salaam na serikali kupitia wizara ya ardhi na nyumba.
Mchezaji huyo pia ameteuliwa nahodha mpya wa timu ya taifa Taifa Stars, nafasi ambayo awali ilishikiliwa na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anayeichezea klabu ya Yanga, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.
Samatta, maarufu ‘Samagoal’ aliwapiku Robert Kadiaba na Bounedjah Baghdad wa Algeria anayeichezea klabu ya Etoile du Sahel na kutwaa tuzo hiyo.
Baada ya kupokea taji lake katika sherehe za kuwatuza wachezaji bora Afrika, mjini Abuja, Samatta alirejea Tanzania na baadaye kualikwa na Rais wa Zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Mnamo mwaka wa 2013, serikali ya Nigeria iliwakabidhi wachezaji wake sehemu ya ardhi mjini Abuja na pesa kwa kushinda kombe la Afcon.
Samatta azawadiwa na serikali ya Tanzania
Reviewed by Ino
on
9:49:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment