Man United imesajili Bastian Schweinsteiger

Manchester United imekubaliana na Bayern Munich kumsajili kiungo cha kati wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger
Kiungo
huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa ameieleza klabu yake kuwa hakutaka
mkataba mpya ambao ungemuongezea muda baada ya mkataba ulioko sasa
kukamilika ifikapo mwisho wa mwaka ujao.Hata hivyo mkurugenzi mkuu mtendaji wa klabu hicho Karl-Heinz Rummenigge amekiri kuwa tayari Manchester United wamewasiliana nao.
''mwenzangu wa klabu ya man united amewasiliana na nami na tayari tumekubaliana nao'' alisema Rummenigge.
Schweinsteiger amecheza mechi 536 tangu ajiunge na klabu hiyo ya Bayern mwaka wa 2002.
Rummenigge "kwa hakika inahuzunisha sana kwani Bastian alikuwa ni kigogo wa timu hii.''

''Kwetu ni heshima kwani ametuhudumia kwa miaka 17 kwa hivyo tukamuacha aendee akastaafie Uingereza'' alisema Rummenigge
Kusajiliwa kwake kunafikisha 3 idadi ya wachezaji waliosajiliwa baada ya mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos, na Muitaliano Matteo Darmian.
Yamkini Kocha Louis Van Gaal anatarajia kuzuru Marekani akiwa na kikosi dhabiti kwa mazoezi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza.
Man United imesajili Bastian Schweinsteiger
Reviewed by Ino
on
11:21:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment