Man United kumsajili Matteo Darmian
Kocha
wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amethibitisha kuwa beki
wa kilabu ya Torino Matteo Darmian atafanyiwa ukaguzi wa matibabu kabla
ya kuhamia kilabu hiyo kwa pauni milioni 12.9.
Mshambuliaji wa
Manchester united Robin Van Persie tayari anaendelea na mazungumzo na
kilabu ya Fenerbahce na Van Gaal anasema:Iwapo tutahisi anaendelea vyema
tutasema,lakini kufikia sasa hatuna hisia hiyo.Kuhusu uhamisho,aliongezea:''Nilisema mwishoni mwa msimu uliopita kwamba ununuzi wa wachezaji na uuzaji ni hatua.Hatua hiyo huendelea hadi mwezi Septemba.''Naona kama uhamisho huo unachukua mda mrefu.Nimesema hivyo mara nyingi.hatahivyo tunaendelea vyema'
Man United kumsajili Matteo Darmian
Reviewed by Ino
on
11:22:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment