Waziri mkuu wa Serbia Vucic apigwa mawe

Waziri
mkuu wa Serbia Aleksandar Vucic,amepigwa mawe na kufukuzwa na raia wa
Bosnia katika hafla ya ukumbusho wa miaka 20 ya mauaji ya halaiki ya
watu katika mji wa Srebrenica
Waziri huyo alilazimika kutorokea maisha yake bada ya kutupiwa chupa mawe na matusi.Mashamblizi hayo yalitokea bwana Vucic alipokuwa akiondoka kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa katika makaburi ya takriban wahanga 136 wa mauaji hayo.

Vikosi vya majeshi ya Bosnia Serb viliwaua wanaume 8000 waisilamu na wavulana wa Srebrenica baada ya kuvamia kambi ambayo ilistahili kulindwa na umoja wa mataifa.
Mauaji hayo yanadaiwa kuwa ndiyo yaliyoisababisha Yugoslavia kuvunjika.

Rais wa zamani wa marekani Bill Clinton ni mmoja wa wale wanaodhuruia maadhimisho hayo.
Awali waziri mkuu Vucic alikuwa ametoa risala za rambirambi japo aliepuka kukiri kuwa yalikuwa mauaji ya halaiki.
Waziri mkuu wa Serbia Vucic apigwa mawe
Reviewed by Ino
on
11:20:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment