Siku ya mwisho ya kuboresha Windows 10 bure
Tarehe 29 mwezi Julai ndio siku ya mwisho kwamba wateja wanaweza kupata kuboresha bure programu ya Windows 10.
Wale watakaoshindwa kuchukua fursa hiyo watalazimika kulipa huku toleo la nyumbani likigharimu dola 120 na lile la kitaalamu likigharimu dola 200.
Vifaa vinavyotumia programu hiyo ni pamoja na pakatalishi na huduma za mawasiliano za kibinafsi.
Kampuni ya Microsoft imekosolewa kwa kutumia uwezo wake bila kujali wateja wake katika kukuza na kuboresha programu hiyo.
Mnamo mwezi Mei ,kampuni hiyo ilishtumiwa kwa kutumia ujanja wakati ilipobadilisha boksi la Pop-up na kuwahamasisha watumiaji wake kuboresha.
Ujanja huo ulibainika wakati mtu anapobofya kuizima programu hiyo ambapo inaendelea kujiboresha badala ya kuzima.
Siku ya mwisho ya kuboresha Windows 10 bure
Reviewed by Ino
on
11:59:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment