Kampuni miliki ya Google yapata faida
Alphabet
Alphabet ambayo ndiyo kampuni mama ya Google imeendelea kupata faida kutokana na wingi wa matangazo ya kibiashara wanayopata, hasa yanayopokelewa na wateja kupitia simu za mkononi.
Kutokana na kushinda zabuni za matangazo hayo ya kibiashara, mapato katika kipindi cha mwezi April hadi Juni yamepanda kwa asilimia 21.3% na kufikia $21.5bn kutoka $17.7bn mwaka uliopita.
Pato la jumla katika miezi mitatu iliyopita yalikuwa $4.9bn, ukilinganisha na $3.9bn katika kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Hisa za Alphabet nazo zimeongeza thamani kwa asilima 6%.Google pia inajipanga kuingia katika biashara ya kuwasilisha ujumbe kupitia video ,washindani wao wakubwa wakiwa Facebook na Twitter.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo , Sundar Pichai, amesema wanataka kutumia vifaa maalum vitakavyo wawezesha kutekeleza mradi wao ambapo Google itaweza kuwapendekezea na kuwaelekeza wateja kwa aina ya video zilizoko YouTube zinazofanana na zile wanazopendelea kutazama.
Mwaka jana Google ilifanya mradi mkubwa wa kujipanga kimkakati na ndipo wakaunda hiyo kampuni mama - Alphabet.
Kampuni miliki ya Google yapata faida
Reviewed by Ino
on
12:04:00 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment