Luis Suarez amepata majeraha katika fainali ya Kombe la Mfalme

Luis Suarez amepata majeraha katika fainali ya Kombe la Mfalme 

Hofu imetanda huenda mchezaji huyo wa taifa wa Uruguay anaweza kukosa fainali za Copa America baada ya kuumia fainali Kombe la Mfalme na nafasi yake kuchukuliwa na Rafinha

Barcelona walipata pigo kwenye mechi ya fainali Kombe la Mfalme baada ya Luis Suarez kutolewa mapema kipindi cha pili kwa sababu ya majeraha.

Wakati matokeo dhidi ya Sevilla bado yakiwa yanasomeka 0-0 mshambuliaji huyo alishindwa kuendelea kucheza vizuri baada ya dakika 56.

Alijitahidi kutembea lakini alikuwa na majeraha katika misuli yake ya paja hivyo kukilazimu kikosi cha Luis Enrique kuendelea bila huduma yake.

Rafinha aliingia kuchukua nafasi yake.

Uruguay sasa watabaki wakisali majeraha hayo yasiwe mabaya kwani mchezaji huyo ni tegemeo kwa taifa lake katika michuano ya Copa America.

 
Majeraha hayo ya misuli kwa yakini yanaweza kumfanya Suarez akose michuano hiyo ya Amerika itakayopigwa kule Marekani kuanzia mwezi Juni.

Luis Suarez amepata majeraha katika fainali ya Kombe la Mfalme Luis Suarez amepata majeraha katika fainali ya Kombe la Mfalme Reviewed by Ino on 10:23:00 PM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.