Uchaguzi TZ:Tume ya uchaguzi yaagiza

   Tume ya Uchaguzi 
 
Huku zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania,tume ya uchaguzi nchini humo imetumia vipengee kadhaa katika sheria kuwaonya wanasiasa na raia wakati wa shughuli hiyo.
Vilevile vyama vya kisiasa na wagombea wametakiwa kuheshimu na kutekeleza sheria za uchaguzi, maadili ya uchaguzi na maelekezo ya tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Sheria zingine za nchi katika kipindi chote cha Uchaguzi.
Kulingana na taarifa iliotumwea kwa vyombo vya habari na mkurugenzi wa tume hiyo Kailima Kombwey vyama vyote vya siasa, wagombea wanachama na wafuasi wa vyama vya siasa wametakiwa kuhakikisha kwamba wanafanya hatua za makusudi kupitia kufanya uchaguzi ulio huru na haki, kukataa na kulaani vitendo vya vurugu na vitisho pamoja na kueneza taarifa sahihi kuhusiana na mchakato wa uchaguzi.
Tume hiyo imesema kuwa watu hawataruhusiwa maeneo ya umbali wa mita 200 kutoka kituo cha kupiga kura baada ya kushiriki katika zoezi hilo ili kutoa fursa kwa raia wengine kupiga kura.
"Hakuna mtu atakayefanya mkutano siku ya kupiga kura au,ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika uchaguzi unaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita miambili lajengo hilo, kuvaa au kuonyesha kadi ya picha yoyote, upendeleo au nembo nyingine inayoonesha kuunga mkono mgombea Fulani katika uchaguzi" tume hiyo ilisema.


 Uchaguzi 
 
Sheria hiyo ya uchaguzi pia inasema kuwa hakuna mtu atakayeruhusiwa, katika jengo lolote ambalo upigaji kura katika uchaguzi unaendelea, au njia yoyote inayotumiwa na umma ndani ya umbali wa mita mia tatu ya mlango wowote wa kuingilia katika jengo. Hivyo tume hiyo inasema kuwa umbali huo wa mita 200 mpaka 300 sio umbali unaowaruhusu watu kukusanyika kwa kisingizio cha kulinda kura.
Imesema kuwa uzoefu unaonyesha kwamba, katika kampeni zinazoendelea, wafuasi wa vyama tofauti wanapokutana uwezekano wa kutokea vurugu ni mkubwa na sehemu nyingine vurugu hutokea na kusababisha maafa majeruhi na uharibifu mali.
Uchaguzi TZ:Tume ya uchaguzi yaagiza Uchaguzi TZ:Tume ya uchaguzi yaagiza Reviewed by Ino on 9:58:00 AM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.