Liverpool waambulia sare Europa League

Klopp amesema hakufurahishwa na matokeo hayo
Meneja mpya wa
Liverpool Jurgen Klopp alishindwa kuandikisha ushindi mechi yake ya
kwanza Anfield baada ya vijana wake kulazimishiwa sare ya 1-1 na Rubin
Kazan katika Europa League.
Wageni wao walichukua uongozi kupitia
Marko Devic lakini nahodha wao Oleg Kuzmin alifukuzwa uwanjani baada ya
kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano muda mfupi baadaye.Liverpool walijibu kupitia Emre Can baada ya kuchapwa kwa frikiki.
Nguvu mpya Christian Beneteke alikosea pembamba kuwafungia la pili baada ya kombora lake kugonga mlingoti wa goli na mwishowe Liverpool wakakubali kuondoka na sare ambayo ndiyo ya tatu mtawalia katika mechi zao Kundi B.
Licha ya kujikakamua sana dakika za mwisho, haukuwa usiku mwema kwa Klopp na Liverpool kwani walishindwa kupenya ngome ya wapinzani wao vipindi virefu vya mechi hiyo.
Matokeo hayo yamewaacha Liverpool nambari mbili katika kundi lao wakiwa na alama tatu, alama nne nyuma ya viongozi FC Sion.
Liverpool sasa wametoka sare mechi saba kati ya nane walizocheza karibuni zaidi.
Akizungumza baadaye, Klopp alisema: "Unapoingia kwenye nyumba mpya, huwa unapokea zawadi. Sijafurahishwa na zawadi niliyoipata leo".
Kwenye mechi nyingine zilizochezwa Alhamisi, matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
Molde 3 - 1 Celtic
Anderlecht 2 - 1 Tottenham Hotspur
Liverpool 1 - 1 Rubin Kazan
Fenerbahçe 1 - 0 Ajax
Monaco 1 - 0 FK Qarabag
Apoel Nic 2 - 1 Asteras Tripolis
Schalke 2 - 2 Sparta Prague
AZ Alkmaar 0 - 1 FC Augsburg
Partizan Belgrade 0 - 2 Athletic Bilbao
Bordeaux 0 - 1 FC Sion
FK Qabala 1 - 3 Borussia Dortmd
Liverpool waambulia sare Europa League
Reviewed by Ino
on
12:16:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment