Wanajeshi waliowaua raia harusini mashakani
Wanajeshi
Kiongozi
mkuu wa jeshi la muungano wa Afrika linalohudumu nchini Somalia,
anasema kuwa wanajeshi watatu wa kikosi hicho wameshtakiwa kuhusiana na
mauaji ya mwezi uliopita ya kundi moja la raia.
Maman Sidikou
aliomba msamaha na akatoa kile ambacho amesema ni rambirambi kwa jamaa
ya watu saba wa familia moja waliopigwa risasi katika mji wa Merka,
kusini mwa mji mkuu Mogadishu.
Kwa mjibu wa kundi moja la kutetea haki za binaadamu- Human Rights Watch, wanajeshi wa umoja wa Afrika kutoka Uganda waliwashambulia kwa risasi watu waliokuwa wakihudhuria harusi baada ya msafara wao kulipuliwa kwa bomu.
Askari hao watahukumiwa katika mahakama ya kijeshi.
Kwa mjibu wa kundi moja la kutetea haki za binaadamu- Human Rights Watch, wanajeshi wa umoja wa Afrika kutoka Uganda waliwashambulia kwa risasi watu waliokuwa wakihudhuria harusi baada ya msafara wao kulipuliwa kwa bomu.
Askari hao watahukumiwa katika mahakama ya kijeshi.
Wanajeshi waliowaua raia harusini mashakani
Reviewed by Ino
on
8:50:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment