Waliom'baka na kumuua msichana wasakwa
Serikali
ya Sierra Leone imetangaza kuwa itampa kitita cha dola $1,000 (£640)
zawadi mtu yeyote atakaye toa habari zitakazofanikisha kukamatwa kwa
genge linalotuhumiwa kum'baka na kumuua msichana aliyekuwa chini ya
miaka 18.
Mwili wa msichana Hannah Bockarie, anayesemekana alikuwa
akifanya kazi ya uchangu doa ulipatikana ufuoni mwa bahari ya eneo la
mji mkuu wa nchi hiyo , Freetown, huku akiwa amejazwa michanga mdomoni
mwake.Jana usiku wanawake wanaotetea haki za binadamu walikusanyika na kuwasha mishumaa wakiomboleza kifo chake.
Wengi wameshtushwa na jinsi alivyouawa kikatili kama picha zilizotandazwa mitandaoni zilivyodhihirisha.
Wanaharakati hao sasa wameanzisha kampeni ya kukemea kitendo hicho na kutaka wahalifu hao kuchukuliwa hatua za kisheria, kampeni hiyo wameipa jina 'mimi ni Hannah".
Waliom'baka na kumuua msichana wasakwa
Reviewed by Ino
on
8:52:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment