Viongozi wa Ulaya kuamua hatima ya Ugiriki

Siku
muhimu ya majadiliano kuhusu madeni ya Ugiriki, imeanza mjini Brussels,
kuamua iwapo Ugiriki itabaki katika umoja wa nchi zinazotumia sarafu ya
euro au la.
Jopokazi, linachambua ombi la Ugiriki, kutaka msaada mpya kabla ya mawaziri wa fedha kukutana.Serikali ya Ugiriki inapendekeza kuchukua hatua kali zaidi za kubana matumizi, kama kuzidisha kodi ya mapato na kuzidisha umri wa kuweza kustaafu.

Mapendekezo hayo yalikubaliwa kwa sauti kubwa katika bunge la Ugiriki, kwenye kikao cha jana usiku.
Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya, wanatarajiwa kujadili mapendekezo hayo ya Ugiriki siku ya jumapili.

Baada ya kikao kilichoendeleka hadi usiku wabunge 252 waliipa serikali idhini ya kufanya mazungumzo na wakopeshaji wake.
Waziri mkuu Alexis Tsipras alishindwa kupata kura za wabunge kumi kutoka chama chake cha Syriza wakiwemo mawaziri wawili wa serikali na spika wa bunge.

Bwana Tsipras alikiri kuwa mabadiliko yaliyopendekezwa yalikuwa nje ya ahadi zilizotolewa na chama chake.
Mapendekezo hayo yatajadiliwa na mawaziri wa fedha wa nchi za ulaya hii leo na pia viongozi wa ulaya kesho jumapili.
Viongozi wa Ulaya kuamua hatima ya Ugiriki
Reviewed by Ino
on
11:15:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment