Maandamano ya umoja yaanza Paris.
Maandamano ya umoja nchini Ufaransa yameanza baada ya makundi ya watu
kukongamana katika eneo la de la Republique katika mji mkuu wa Paris
nchini Ufaransa ,kama kigezo cha kuonyesha umoja dhidi ya mashambulizi
ya wiki iliopita yaliotekelezwa na waislamu wenye itikadi kali.
Zaidi ya watu millioni moja wanashiriki katika maandamano hayo.Makumi ya viongozi wa nchi tofauti duniani wako mji paris ambapo usalama umeimarishwa huku maafisa zaidi wa jeshi na wale wa polisi wakiwekwa kupiga doria.
Ghasia hizo nchini Ufaransa zilianza siku ya jumatano kutokana na shambulizi la gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Hatahivyo maafisa wa polisi waliwazingira na kuwapiga risasi mandugu wawili waliohusika na shambulizi hilo.
Maandamano ya umoja yaanza Paris.
Reviewed by Ino
on
9:25:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment