Bony kuhamia Mancity kwa £30m
Kilabu ya Uingereza Swansea City imekubali ada ya uhamisho ya takriban
pauni milioni 30 kutoka kwa Manchester City ya kumnunua Wilfried Bony,
26.
Meneja wa Swansea, Gary Monk amesema kuwa itahitaji "kitita cha ajabu" kumhamisha Bony kutoka Swansea.
Bony alijiunga na Swansea mwaka 2013 kutoka Vitese Arnhem kwa pauni milioni 12.
Mchezaji huyo kwa sasa yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Bony kuhamia Mancity kwa £30m
Reviewed by Ino
on
9:26:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment