Wenger:Safu ya ulinzi ilikuwa maji maji.

Safu
ya ulinzi ya Arsenal ilikuwa ''maji maji'' sana dhidi ya Stoke wakati
timu hiyo ilipolazwa kwa mabao 3-2 katika uwanja wa Bitania ,kocha
Arsena wenger amesema.
The Gunners ilifungwa mabao matatu katika kipindi cha kwanza ,ikiwemo bao kwanza baada ya sekunde 19 kabla ya kuanza kuvamia lango la Stoke ili kulipiza.
Nadhani tulikuwa hatuna uzoefu wa siku nyingi katika safu ya nyuma,alisema.

Koscielny aliyeanza mechi mbili zilizopita alipumzishwa huku Monreal akiwa na jeraha.
Kierran Gibs alicheza kama beki wa kushoto naye calum Chamber akisaidiana na Per Mertesacker katika safu ya Ulinzi huku mchezaji mwenye umri wa miaka 19 hector Bellerin akianzishwa kama beki wa kulia.
Wenger:Safu ya ulinzi ilikuwa maji maji.
Reviewed by Ino
on
11:48:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment