Nigeria na USA kukutana katika dimba

Timu za wanawake zikiminyana katika dimba la dunia lilopita.
Canada 2015: Nigeria yapangwa na USA katika kundi gumu la Kombe la Dunia Mabingwa wa Africa; Nigeria wamepangwa katika kundi la kifo la Kombe la dunia la wanawake mwaka 2015 Canada.

Nigeria itachuana na mabingwa wa Olimpiki Marekani katika kundi D katika fainali za za kombe la dunia zitakazochezwa kati ya Juni 6 na Julai 5.
Timu hiyo inayojulikana kama "Super Falcons" pia itachuana na Sweden na Australia katika kundi D mjini Winnipeg.
Kwengineko Ivory Coast itacheza machi zake mjini Ottawa, katika kundi B pamoja na Ujerumani , Norway na Thailand.
Cameroon - taifa la tatu la Afrika kushiriki litachuana na Japan, Switzerland na Ecuador mjini Vancouver.
Hivi ndivyo michuano hiyo ilivyopangwa, . 2015 World Cup draw
Group A Canada China New Zealand Netherlands
Group B Germany Ivory Coast Norway Thailand
Group C Japan Switzerland Cameroon Ecuador
Group D USA Australia Sweden Nigeria
Group E Brazil South Korea Spain Costa Rica
Group F France ENGLAND Colombia Mexico
Nigeria na USA kukutana katika dimba Nigeria na USA kukutana katika dimba Reviewed by Ino on 11:49:00 AM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.