Ebola:Hofu ya maambukizi zaidi

Shirika
la afya duniani limetahadharisha kuwa linatarajia kuona maambukizi
zaidi ya Ebola licha ya kile linachosema ni kuongeza kasi juhudi za
kupambana na janga hilo katika wiki chache zilizopita.
Msemaji wa shirika hilo, Daktari, Chris Dye, anasema kuwa wagonjwa katika maeneo yaliyoathirika zaidi ,Guinea, Sierra Leone na Liberia kuna uhaba wa vitanda
Mojawapo ya mashirika yanayoongoza vita dhidi ya ebola huko Afrika magharibi limesema ulimwengu hauna budi kuchapuza harakati za kuzuia janga hilo.

MSF linasema kumekuwa na ongezeko kubwa katika mji mkuu wa Guinea, Conakry, ongezeko linaloondosha matumaini kwamba maambukizi ya Ebola yanadhibitiwa .

Rais Conde anasema nchi yake inahitaji mambo kadhaa ili kuimarisha vita dhidi ya Ebola.
Kwingineko nchini Uhispania, watu 7 zaidi wamo katika uangalizi hospitalini kuona iwapo wameathirika na Ebola.

Kwa sasa ni yuko katika hali mahututi, na anaarifiwa yumo katika hatari ya kufariki.
La kutia moyo ni kuwa muuguzi mmoja nchini Austarlia aliwekwa kwenye karantini na kufanyiwa uchunguzi wa maabara amegunduliwa hana Ebola.
Waziri wa usalama wa ndani Marekani, Jeh Johnson amesema anataka nchi zaidi kuidhinisha ukaguzi wa virusi hivyo katika viwanja vya ndege vya kimataifa kuzuia kuenea kwake.
Ebola:Hofu ya maambukizi zaidi
Reviewed by Ino
on
7:15:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment