TP Mazembe nje Klabu Bingwa Afrika

Timu
Entente Setif ya Algeria sasa itapambana na AS Vita Club ya Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo katika fainali ya Klabu Bigwa barani Afrika baada
ya kuiondoa TP Mazembe pia ya Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo kwa
faida ya magoli ya ugenini japo TP Mazembe ilishinda hapo jana mechi ya
nusu fainali kwa magoli 3 - 2.Entete Setif na TP Mazembe zote zilimaliza nusu fainali kila moja ikiwa na magoli manne kwa manne,magoli mawili Setif iliyoyafunga ugenini imewasaidia kuwa timu iliyofunga magoli mengi ikiwa ugenini.
Nayo AS Vita Club imetinga hatua hiyo fainali baada ya kuibamiza CS Sfaxien ya Tunisia siku ya jumamosi kwa ushindi wa jumla wa magoli 4 - 2.
Hata hivyo mashabiki TP Mazembe pamoja na timu yao kutolewa katika mashindano hayo ambayo sasa itachezea mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wamesema wataiunga mkono AS Vita Club ambayo ni timu nyingine kutoka DRC.
TP Mazembe nje Klabu Bingwa Afrika
Reviewed by Ino
on
1:45:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment