Man united yamnunua Di Maria

Man united yamnunua Di Maria 

Manchester United imekubali kumchukua Winga wa Real Madrid
Anji di maria kwa pauni milioni 59.7 nakuvunja rekodi ya kiwango cha fedha kwa wachezaji wanaonunuliwa kuchezea timu za England.
Di Maria mwenye umri wa miaka 26, yuko jijini Manchester na anatarajiwa kufanya vipimo vyake vya kiafya asubuhi hii.
Mchezaji huyo pengine ataungana na kikosi cha Man United katika mchezo wa ligi kuu ya England utakaofanyika siku ya jumamosi dhidi ya Burnley
Mchezaji huyo ndiye aliyegharimu kitita kikubwa zaidi katika historia ya ligi kuu ya Uingereza
Kitita kilichotolewa kwa ajili ya Muajentina Di Maria kimezidi kiwango cha pauni milioni 50 ambacho kilitolewa na Chelsea kumnyaka Fernando Torres mwaka 2011.
Manchester United imeshawanunua wachezaji kama beki wa kushoto Luke Sho,Kiungo wa kati Ander Herrera na Muajentina Marcos Roho kwa jumla ya Pauni milioni 72 kipindi hiki cha majira ya joto.
Man united yamnunua Di Maria Man united yamnunua Di Maria Reviewed by Ino on 10:15:00 PM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.