IS ilikiuka haki za kibinadamu Syria

Ripoti ya UN imesema kuwa IS ilikiuka haki za kibinadamu Syria
Umoja wa Mataifa umewashtumu
wanamgambo wa Islamic State kwa kuwahujumu watu mara kwa mara mbali na
kuwasajili watoto kuhudumu kama wanajeshi.Wakati huohu UN imeistuhumu serikali ya Syria kwa kutumia kemikali aina ya Chlorine katika matukio manane katika ripoti mpya kuhusu uhalifu wa vita nchini humo.
Islamic State ambayo kwa sasa inadhibiti sehemu kubwa ya Syria ni moja ya vikundi ambavyo vinapigana na serikali ya rais wa Syria ,Bashar al-Asaad.
Zaidi ya watu laki mbili wameuawa tangu vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe kutibuka mwaka wa 2011.

Watoto walilazimishwa kujiunga na jeshi la IS
Ripoti hiyo inaeleza kwamba miili ya wale walio uawa huwa inawekwa kwa maonyesho kwa siku kadhaa kitu ambacho hutishia wakaazi wa huko.
Aidha wanawake wamepigwa kwa kutovalia hijabu huku wale wanaoshtumiwa kwa usherati wakipigwa mawe hadi kufa hadharani.
Mjini wa Raqqa, watoto wachanga wenye umri wa miaka 10 wanapewa mafunzo katika kambi za IS.

Serikali ya Syria nayo ilitumia kemikali mara 8
Wachunguzi hao walionya kuwa vita hivyo vinakila dalili ya kuenea kwa mataifa yaliyoko karibu.
Mmoja wa wachunguzi hao wa kimataifa Carla del Ponte, ameoamba jamii ya kimataifa kuishatki Syria katika mahakama ya ICC kama vile ilivyofanya dhidi ya Rwanda.
IS ilikiuka haki za kibinadamu Syria
Reviewed by Ino
on
5:43:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment