Wakombozi wa vita wamrushia Mugabe maneno makali
Serikali ya Zimbabwe imekashifu vikali hatua ya baadhi ya ma-veterani wa vita vya ukombozi nchii humo ya kumrushia maneno makali rais wa nchi hiyo Robert Mugabe.
Serikali imetaja kitendo hicho kama usaliti , wakisema watawachukulia hatua wote waliohusika na kuandikwa kwa taarifa iliyotolewa na maveterani hao wakimsema rais Mugabe ni dikteka aliyeuangusha uchumi wa Zimbabwe.
Kabla ya matukio haya ya sasa Maveterani hao walikuwa wakimuunga mkono Mugabe kwa dhati tangu nchi hiyo ilipojinyakulia uhuru wake katika miaka ya 70, kwani ndio waliomsaidia kushika usukani wa madaraka nchini humo.
Sasa wanasema hawatamuunga mkono Mugabe mwenye umri wa miaka 92 ambae anataka kuwania muhula mwengine tena hapo 2018.
Kumekuwa na ongezeko la maandamano ya kupinga utawala wa Mugabe mnano siku za hivi karibuni kutokana hasa na kuendelea kwa mdororo wa kiuchumi, dolla ya Zimbabwe kusambaratika,na kufikia kiwango cha hadi serikali kushindwa kuwalipa wafanyikazi wake.
Wakombozi wa vita wamrushia Mugabe maneno makali
Reviewed by Ino
on
12:14:00 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment