Kutizama Tv kunaweza kukuua, utafiti

Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Japan umethibitisha kwamba kukaa kwa mda mrefu na kutazama vipindi vya televisheni kwa masaa mengi kunahatarisha afya kwani huhusishwa na maradhi yanasababisha mzunguko wa damu mwilini kutokuwa sawa.
Watafiti hao wanasema, hali hiyo pia huenda ikasababisha damu kuganda na kutengeneza vidonge katika sehemu kama vile miguu, na iwapo mgando huo utasukumwa na nguvu za mzunguko wa damu na kuingia sehemu kama vile mapafu, husababisha vifo.
Utafiti huo ulihusiha watu zaidi ya 86,000 ambao hupendelea kutazama televisheni katika mida mbalimbali kwa siku.
Kisha afya zao zilifuatiliwa kwa zaidi ya miaka 19 tangu mwaka 1988 hadi 1990.

Matokeo yalikuwa kila muda wa masaa mawili yalipopita mtu akikaa kutazama televisheni, nayo hatari ya kupata ugonjwa huo wa mapafu uitwao ‘Fatal pulmonary embolism’ ulioongezeka kwa asilimia 40%.
Iligundulika pia kuwa waliotazama vipindi vya televisheni kwa zaidi ya saa 5 walikuwa katika hatari zaidi kuliko waliotazama televisheni kwa mda wa chini ya saa 3.
Zaidi ya hayo watu huambatanisha kitendo cha kukaa na kutazama televisheni huku wakila vitafunio kama vile Popcorns na Crisps ambavyo pia huwasababishia si tu mwili kukosa mazoezi bali pia kuongezeka kwa uzito unaohatarisha afya.
Kutizama Tv kunaweza kukuua, utafiti Kutizama Tv kunaweza kukuua, utafiti Reviewed by Ino on 9:14:00 AM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.