Liverpool yamsaka Sadio Mane

Liverpool imeanza kumwinda mshambuliaji wa Southampton Sadio Mane katika uhamisho wa kitita cha pauni milioni 30.
Liverpool na Southampton zitaendelea kufanya mazungumzo kuhusu mpango huo huku kitita hicho cha uhamisho kikiwa swala muhimu.
Southampton wanadaiwa kutaka pauni milioni 40 kwa mchezaji huyo ambaye alifunga mabao 11 katika mechi 37 alizocheza msimu uliopita.
Kitita hicho ni pauni milioni 10 zaidi ya kile kinachopendekezwa kutolewa na Liverpool swala ambalo litahitaji mazungumzo zaidi kabla ya mpango huo kuidhinishwa.
Southampton vilevile iko katika harakati za kumsajili mrithi wa Ronald Koeman aliyeelekea kujiunga na klabu ya Everton hatua ambayo huenda ikachelewesha mpango huo.

Jurgen Klopp
Liverpool yamsaka Sadio Mane
Reviewed by Ino
on
2:22:00 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment