Manchester United yamfuta kazi Louis van Gaal

Louis Van Gaal
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester
United Louis van Gaal amefutwa kazi kama mkufunzi wa klabu ya Manchester
United, huku aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa
kuchukua mahala pake.
Kitengo cha habari za michezo cha BBC Sport kiliripoti siku ya Jumamosi kwamba ushindi wa United wa kombe la FA dhidi ya Crystal palace utakuwa mechi yake ya mwisho akiwa mkufunzi.
Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa baada ya raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 kukutana na maafisa wakuu wa United siku ya Jumanne.
Manchester United yamfuta kazi Louis van Gaal
Reviewed by Ino
on
1:02:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment