Leo ni kivumbi New York

Wagombea wa Democrat Hillary Clinton na Bernie Sanders.
Wagombea waliobaki kwenye
kinyanganyiro cha kuwania urais nchini Marekani, wanang'ang'ania kura
muhimu zaidi za mchujo hii leo katika jimbo la New york, likiwa moja ya
majimbo makubwa nchini Marekania lina ushawishi mkubwa kwa wagombea
wote.
Kwa upande wa Republican mgombea mkuu Donald Trump ni mwenyeji wa jimbo hilo.
Ananuia kupata ushindi dhidi ya mshindani wake mkuu Ted Cruz, Lakini amekosoa mbinu ya kumchagua mgombea wa chama.

Wagombea wa Republican Donald Trump na Ted Cruz
Mshindani wake mkuu Ted Cruz hatarajiwi kufanya vyema baada ya kukosoa sera za Trump mapema kwenye kampeni.
Leo ni kivumbi New York
Reviewed by Ino
on
11:38:00 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment