Choo kinachojifungua na kujiosha
Choo hicho kinauzwa $9,800
Choo cha kisasa
ambacho kina uwezo wa kujifungua unapokaribia na pia kujiosha, ni moja
ya vitu vinavyoonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya teknolojia mpya
za bidhaa za elektroniki Las Vegas.
Choo hicho, kilichopewa jina Neorest, pia humsafisha anayekitumia kwa kifaa kinachotoa maji moto na hewa mtu akiwa ameketi.Kina pia teknolojia inayokiwezesha kuua bakteria na virusi.
Licha ya choo hicho kuuzwa $9,800 (£6,704), waliotengeneza choo hicho vyoo zaidi ya 40 milioni vya miundo ya awali vimeuzwa.
Kampuni ya Toto, iliyotengeneza choo hicho, imesema muundo huo wa sasa bado unaendelea kuboreshwa.
"Huhitaji kuosha bakuli la choo kwa kipindi cha mwaka mmoja,” anasema msemaji wa Toto, Bi Lenora Campos.

Maonyesho hayo ambayo kwa Kiingereza yanajulikana kama Consumer Electronics Show hufanyika kila mwaka ambapo kampuni mbalimbali na wavumbuzi huonyesha teknolojia za karibuni zaidi.
Choo kinachojifungua na kujiosha
Reviewed by Ino
on
9:48:00 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment