Djilobodji aachwa nje ya kikosi cha Chelsea

Papy Djilobodji
Mchezaji
aliyesajiliwa hivi majuzi na Chelsea, Papy Djilobodji, ameachwa nje ya
kikosi cha klabu hiyo kitakachocheza mechi ya ligi ya klabu bingwa
Ulaya, hatua ya makundi.
Mlinzi huyo Djilobodji,mwenye umri wa
miaka 26, kutoka Senegal, alisajiliwa na 'the Blues' siku ya mwisho ya
kuhama wachezaji kutoka klabu ya Nantes ya Ufaransa kwa £4m.Wachezaji wenzake waliojiunga majuzi na mabingwa hao wa Uingereza, Asmir Begovic, Abdul Rahman Baba, Pedro na Radamel Falcao wote wamejumuishwa kwenye kikosi hicho cha wachezaji 25.
Nyota huyo aliachwa nje kwa kuwa Chelsea, walikuwa tayari wamejaza nafasi za wachezaji ambao sio wazaliwa wa Uingereza kwenye kikosi chao cha kwanza.
Mlinda lango wa Manchester United David De Gea, yumo kwenye kikosi cha kilabu hiyo baada ya mpango wa kuhamia Real Madrid kutibuka.
Djilobodji aachwa nje ya kikosi cha Chelsea
Reviewed by Ino
on
6:44:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment