Korea Kaskazini yaitishia Korea Kusini

Huku
msukosuko ukiendelea kushuhudiwa katika rasi ya Korea, Korea kusini
inasema kuwa Korea Kaskazini imepeleka silaha kwenda kwa mpaka baada ya
kutoa vitisho vya kuharibu vipasa sauti vinavyotangaza propaganda kutoka
Korea kusini.
Muda wa mwisho uliotangazwa na Korea Kaskazini wa
kutaka kuondolewa kwa vipasa sauti hivyo unatarawajiwa kukamilika saa
chache zinazokuja.
Korea Kusini inasema kuwa itajibu vikali . Ndege zake za kivita zimekuwa zikiruka pamoja na za Marekani karibu na mpaka.
Mwandishi wa BBC nchini Korea Kusini anasema kuwa ni muda uliotangazwa na korea kaskazini ndio unaoifanya hali kuwa hatari zaidi.
Korea Kaskazini yaitishia Korea Kusini
Reviewed by Ino
on
12:10:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment