Ban aitaka ulaya kuwasaidia wahamiaji

Katibu mkuu wa
Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ametoa wito kwa serikali zote
zinazolishughulikia suala la wakimbizi barani ulaya kutenga maeneo
salama kwa wahamiaji na kuonyesha utu.
Ban amesema kuwa idadi
kubwa ya wakimbizi na wahamiaji ni ishara ya matatizo makubwa kama ya
vita vilivyo nchini Syria ambapo ametoa wito kwa jamii ya kimataifa
kuonyesha moyo wa kutatua mizozo kama hiyo.
Mapema umoja wa mataifa uliwataka viongozi wa nchi za ulaya kuzuia vifo vya wahamiaji baada ya mamia kuaga dunia siku tatu zilizopita.
Ban aitaka ulaya kuwasaidia wahamiaji
Reviewed by Ino
on
2:59:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment