Wakimbizi:UNHCR yaahidi kushirikiana na Kenya
Shirika
la umoja wa mataifa linalosimamia wakimbizi UNHCR limesema kuwa liko
tayari kufanya kazi na serikali ya Kenya ili kuhakikisha kuwa sheria za
Kenya zinafuatwa kikamilifu katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab karibu
na mpaka wake na Somalia.
Shirika hilo limeitaka serikali ya Kenya
kufikiria upya kauli hilo la kuwafurusha wakimbizi na kufunga kambi
hiyo katika kipindi cha miezi tatu ijayo.Serikali ya Kenya ilitoa amri hiyo punde baada ya wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabaab kuwaua wanafunzi wakristu takriban 150 katika chuo kikuu cha Garissa mapema mwezi huu.
Makamu wa Rais William Ruto alitangaza kuwa angetaka wakimbizi hao warejeshwe makwao na kambi hiyo ya Dadaab ifungwe.
Kambi hiyo yenye wakimbizi takriban nusu milioni ndio kubwa zaidi duniani ikiwa na asilimia kubwa ya wakimbizi kutoka Somalia.
Serikali ya Kenya imesema inaushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa asilimia kubwa ya mashambulizi yanayotekelezwa nchini Kenya na kundi la waislamu la Al Shabaab yanapangiwa katika kambi hiyo ya Dadaab.
Haswa ikiashiria shambulizi la maduka ya kifahari ya Westgate ambapo ilidaia washambulizi waliingia nchini kama wakimbizi.
UNHCR inapinga madai hayo.
UNHCR inasema kuwa Kenya itakuwa inakiuka wajibu wake wa kuhakikishia wakimbizi usalama wao pindi wapoingia katika mipaka yake.
Serikali ya kenya kwa ushirikiano na UNHCR na serikali ya Somali iliweka mipango ya kurejesha wakimbizi makwao mwaka uliopita lakini mkataba huo ulikuwa utekelezwe kwa hiari.
Idadi ndogo sana ya wakimbizi hao walikubali kurejea makwao.
Wakimbizi:UNHCR yaahidi kushirikiana na Kenya
Reviewed by Ino
on
8:53:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment