Raia wa Burundi waandamana dhidi ya rais
Polisi
nchini Burundi wamerusha mabomu ya kutoa machozi na maji, ili
kuwatawanya mamia ya waandamanaji katika mji mkuu Bujumbura.
Maandamano
hayo ni ya kumpinga Rais Pierre Nkurunziza, kutowania tena kiti cha
Urais katika uchaguzi mkuu ujao, unaopangiwa kufanyika mwezi Juni.Mwaandishi wa BBC mjini Bujumbura, anasema kuwa malori makubwa yanayobeba vitoa machozi yamewekwa tayari kukabiliana na waandamanaji hao kote katika mji huo.
Anasema kuwa wazazi wamekimbia shuleni ili kuwaondosha watoto wao na kuwapeleka nyumbani.
Bwana Nkurunziza hajasema hadharani iwapo atawania kiti cha urais kwa muhula mwingine, lakini kuna tetesi kuwa ana mpango wa kufanya hivyo.
Raia wa Burundi waandamana dhidi ya rais
Reviewed by Ino
on
11:44:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment