Google yazindua huduma mpya ya simu



Huduma ya Project Fi

Kampuni ya Google imatangaza kuwa itazindua huduma mpya nchini Marekani ambayo inaweza kutumiwa nyumbani na wakati wa safari za mataifa ya kigeni.
Huduma hiyo inayo fahamika kama Project Fi inatapatikana kwa simu za Smartphone za Google Nexus 6.
Huduma hiyo itatumia maeneo yaliyo na Wi-Fi sambamba na huduma zingine za mawasilianoi nchini Marekani za Sprint na T-Mobile na inaweza pia kutumiwa kwenye nchi 120 bila malipo ya ziada wakati mtu anaposafiri nje ya nchi.
Huduma hiyo itatolewa kwa malipo ya dola ishirini kwa mwezi kwa huduma za kawaida na dola kumi kwa mwezi kwa kila gigabyte ya data inayotumika.
Google inasema kuwa huduma hiyo huwa inajiunga moja kwa moja na zaidi maeneo milioni yenye huduna za Wi-Fi na mteja ana uwezo wa kuhamiswa kutoka kwa mtandao mmoja hadi mwingine kulingana na ni upi unaotoa huduma bora zaidi.
Google yazindua huduma mpya ya simu Google yazindua huduma mpya ya simu Reviewed by Ino on 11:24:00 AM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.