Polisi wavunja maandamano Mynmar
Polisi
wa kupambana na ghasia wametumia vitoa machozi kuutawanya umati wa
wanafunzi uliokuwa ukiandamana kupinga sheria mpya wanayosema
inakandamiza uhuru wa elimu.
Walioshuhudia wameiambia BBC kuwa wanafunzi kadhaa wamekamatwa baada ya muafaka wa makubaliano ulioapangwakati ya wanafunzi na wakuu wa elimu kuvunjika na waandamanaji wakijaribu kuvunja vizuizi vilivyowekwa na maofisa wa polisi.
Zaidi ya wanafunzi wapatao 150 walizuiwa katika mji wa Letpadan katika kati mwa Nchi hiyo tangu juma lililopita, baada ya maandamanao yao ya kuufikia mji wa Yangon.
Wanafunzi hao wamezuiwa na polisi wa kupambana na ghasia.
Maandamano hayo ya kupinga sheria hizo mpya ya Elimu yalianza mji wa Mandalay yapata mwezi mmoja uliopita.
Polisi wavunja maandamano Mynmar
Reviewed by Ino
on
5:50:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment