Mtoto wa wazazi watatu kuzaliwa UK

Wanasayansi na maajabu yao
Wabunge wa bunge la Uingereza wameunga mkono sheria inayoruhusu uzaaji wa wa watoto wenye vinasaba, DNA kutoka kwa wanawake wawili na mwaume mmoja, katika tukio la kihistoria.
Uingereza kwa sasa itakuwa nchi ya kwanza kuweka sheria zinazoruhusu watoto wenye vinasaba vya watu watatu tofauti.
Katika kura iliyopigwa katika bunge la Commons, wabunge 382 waliunga mkono muswada huo wa sheria na wabunge 128 walipinga mbinu inayozuia magonjwa ya kijenetiki kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Wakati wa mjadala huo, mawaziri wamesema mbinu hii ni "mwanga kwa safari ndefu ya giza" kwa familia kupata watoto.
Upigaji kura zaidi unahitajika katika baraza la bunge la juu, maarufu kama House of Lords. Iwapo kila kitu kitakwenda sawa, basi mtoto wa kwanza wa teknolojia hii atazaliwa mwaka ujao.
Watetezi wa mpango huu wanasema uungwaji mkono wa sheria hii "ni habari njema kwa maendeleo ya tiba" lakini wakosoaji wanasema wataendelea kupinga mpango huu ambao una mashaka mengi kuhusu maadili na usalama katika uzazi huu.
Makisio yanasema watoto 150 wanaopatikana kutokana na vinasaba vya watu watatu watazaliwa kila mwaka.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron anasema: "Hatuzungumzii Mungu hapa, tunahakikika kuwa wazazi wawili ambao wanataka mtoto mwenye afya wanaweza kumpata."
Mpango huu ambao umebuniwa Newcastle, utasaidia wanawake kama Sharon Bernardi, kutoka Sunderland, ambaye alipoteza watoto wote saba kutokana na ugonjwa wa mitochondrial.
Mtoto wa wazazi watatu kuzaliwa UK Mtoto wa wazazi watatu kuzaliwa UK Reviewed by Ino on 2:24:00 AM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.