Tanzania kuhodhi ligi ya mpira wa wavu
Tanzania
imechaguliwa tena kuwa wenyeji wa michuano ya mpira wa wavu ya mataifa
ya Afrika (All Africa Games) itakayofanyika mapema mwezi wa nne mwaka
huu.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa shirikisho la mpira wa wavu
nchini (Tava) kuchaguliwa kuwa wenyeji wa michuano mikubwa barani Afrika
kwa nchi za ukanda wa tano.Tanzania, kati kati ya mwezi ujao (Februari 16-18) itakuwa wenyeji wa michuano ya mpira wa wavu kwa nchi za kanda ya 5 Afrika na kwa mujibu wa Rais wa Tava, Augustino Agapa, wanajiandaa pia kualika timu kwa ajili ya michuano hiyo ya mataifa ya Afrika.
“ Hivi karibuni nilikuwa Misri katika mkutano wa marais wa vyama vya wavu kutoka nchi za kanda ya 5 na tumepewa heshima ya kuwa wenyeji”, alisema Agapa.
Tanzania kuhodhi ligi ya mpira wa wavu
Reviewed by Ino
on
12:46:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment