Luis Figo atangaza kuwania urais FIFA

Luis Figo mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno Luis Figo ametoa taarifa za kushitusha baada ya kutangaza kuwania Uraisi wa FIFA.
Nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Sporting Lisbon, Barcelona, Real Madrid na Inter Milan mwenye miaka 42 anaungana na mchezaji mwingine wa zamani wa Ufaransa David Ginola katika kuwania nafasi ya kumng'oa madarakani bosi wa sasa Sepp Blatter katika chombo hicho kikubwa cha soka duniani.
Wengine wanaowania kiti hicho mpaka sasa ni Mfalme Ali wa Jordan, Michael van Praag na Jerome Champagne.
Blatter amekuwa kiongozi wa shirikisho hilo tangu mwaka 1998 na akitaka kuendelea kuwania tena uongozi katika awamu ya tano.
Wagombea wote wanaowania kiti hicho wanatakiwa kujiandikisha kabla ya siku ya mwisho ambayo ni Alhamisi.
Kwa mujibu wa mjumbe wa kamati ya uchaguzi Dominico Scala, wagombea wote wanatakiwa kupitishwa na kamati ya FIFA ya kuzuia rushwa michezoni.
Figo ameichezea timu ya taifa ya Ureno mara 127 na aliwahi kutwaa ubigwa wa Ulaya akiwa na Real Madrid 2002.
Mwaka 2000 aliweka rekodi ya uhamisho wa kiasi cha pauni milioni 37 baada ya kuhama Barcelona kwenda Real Madrid.
Pia aliwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mwaka 2000 na mwaka 2001 akatwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka inayotolewa na Fifa.
Luis Figo atangaza kuwania urais FIFA Luis Figo atangaza kuwania urais FIFA Reviewed by Ino on 9:40:00 AM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.