Michuano Kriketi Afrika nchini Tanzania
Michuano
ya kimataifa ya mchezo wa kriketi kwa wanawake chini ya miaka 19,
imeanza kutimua
vumbi kwenye viwanja vya Gymkhana na Annadil jijini Dar
es salaam Tanzania. Mashindano haya yanazishirikisha nchi sita ambazo
ni wenyeji Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya, Botswana, pamoja na
msumbiji.Mchuano hii itafanyika kwa mara ya pili jijini Dar es saalam kwa Tanzania kuwa wenyeji.Michuano hii itachukua muda wa siku tatu kuanzia leo mpaka tarehe 9/12/2014 ambapo itakua tamati ya michuano. Uganda ndio wanalishikilia kombe hilo Kwa kuwa mabigwa watetezi wa michuano hii ya kimataifa ya kriketi kwa wanawake chini ya miaka 19.
Michezo iliyochezwa mapema leo kwenye uwanja wa Annadil Kenya waliwafunga Botswana kwa mikimbio 109 dhidi 97.katika mchezo wa pili Kenya wakawabugiza Rwanda kwa mikimbio 94 kwa 31 na mchezo wa mwisho Rwanda wamewabanjua Botswana kwa mikimbio 68 dhidi ya 67 ……
Kwenye uwanja wa Gymkhana mchezo wa kwanza ulishudia msumbiji akiadhibiwa na Uganda kwa mikimbio 103 dhidi ya 29.Huku wenyeji Tanzania wakiwachapa msumbiji kwa mikimbio 100 kwa 34 na mchezo wa mwisho Tanzania wameambulia patupu kwa kufugwa kwa mikimbio 65 kwa 63 dhidi ya Uganda.
Michezo hiyo itaendelea tena kesho mchezo wa mapema asubuhi kwenye uwanja wa Gymkhana utawakutanishana Kenya na Msumbiji,mchezo wa pili utakua kati ya Tanzania na Kenya, mchezo wa mwisho wenyeji Tanzania watachuana na Rwanda.
Wakati kwenye uwanja wa Annadil mchezo wa kwanza Uganda watachuana na Rwanda,mchezo wa pili Botswana watapepetana na Uganda, na mchezo wa mwisho utawakutanisha Botswana dhidi ya Msumbiji.
Michuano Kriketi Afrika nchini Tanzania
Reviewed by Ino
on
9:15:00 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment