Henry ataka kuisaidia Arsenal
Uwezekano
wa Thiery Henry kujiunga na Arsenal kama mkufunzi umeongezeka baada ya
mchezaji huyo wa Ufaransa kufichua kwamba bado ana ndoto ya kuisadia
Arsenal kushinda taji la kilabu bingwa barani Ulaya.
Henry huenda akaweka viatu vyake vya soka chini jumamosi wakati ambapo kilabu yake ya New York Red Bulls itajaribu kulipiza kichapo cha mabao 2-1 ugenini katika fainal ya raundi ya pili dhidi ya New England Revolution.
Mchezaji huyo mwenye miaka 37 amekamilisha kandarasi yake na kilabu hiyo na ijapokuwa anasema kuwa hakuna kilichoafikiwa kuhusu hatma yake ameanza kutoa maoni yake kuhusu maisha yake baada ya kusakata soka.

''hakuna kilicho wazi''Henry aliliambia gazeti la L'Equipe.''Sijafanya uamuzi wowote na mimi sipendelei uvumi'',.
''Kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba nitasalia katika soka kama mkufunzi ama afisa mkuu ,lakini tutaona'',alisema.
Henry ataka kuisaidia Arsenal
Reviewed by Ino
on
11:33:00 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment