Jules Bianchi apata ajali

Jules Bianchi
Katika Mashindano ya mbio za magari ya langa langa ya Formula One dereva wa Ufaransa, Jules
Bianchi, yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuumia vibaya kichwa chake kutokana na ajali ya kugongana na dereva mwingine katika mashindano ya Japan Grand Prix. Madaktari wa upasuaji wanaendelea kumhudumia dereva huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alipoteza fahamu wakati alipofikishwa hospitalini hapo.Bianchi alipoteza uelekeo wa gari lake kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, hata hivyo ajali hiyo iliyosababishwa na mwendo kasi mkubwa.Dereva wa Uingereza Lewis Hamilton alitangazwa mshindi katika mashindano hayo.
Jules Bianchi apata ajali Jules Bianchi apata ajali Reviewed by Ino on 10:07:00 PM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.