England yaikomoa San Marino 5-0

Timu
ya England imefanikiwa kupata ushindi mara mbili katika michezo miwili
ya kundi E ya kufuzu kucheza michuano ya bara la Ulaya ya mwaka 2016
baada ya kupata ushindi mnono wa 5-0 dhidi ya San Marino.
England alianza kuvuna magoli kupitia kwa mlinzi wake Phil Jagielka aliyefunga katika dakika ya 24 kwa mpira wa kichwa kabla ya Wayne Rooney kuongeza bao la pili kwa njia ya penalti katika dakika ya 43 kutoka na madhambi ya mchezaji wa San Marino Andy Selva.
Naye mshambuliaji Danny Welbeck alifanikiwa kutumbukiza goli la tatu kwenye dakika ya 49. Goli hili lilitokana na mpira wa pasi kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Arsenal ambaye aliingia kipindi cha pili Alex Oxlade-Chamberlain.
Andros Townsend aliiongezea timu yake ya England goli la nne kwa mkwaju wa mbali kabla ya Alessandro Della Valle kujifunga mwenyewe kutokana na kugongwa na mpira uliopigwa na Rooney.
Matokeo ya michezo mingine: Belarus 0: Ukaraine 2, Macedonia 3: Luxembourg 2, Slovakia 2: Spain 1, Lithuania 1:Estonia 0, Slovenia 1: Switzerland 0, Liechtenstein 0: Montenegro 0, Moldova 1:Austria 2, Sweden 1: Russia 1
England yaikomoa San Marino 5-0
Reviewed by Ino
on
7:03:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment