WHO:Visa vya Ebola vimeongezeka kwa kasi
Shirika la
afya duniani WHO linasema kuwa idadi ya visa vipya vya ugonjwa wa Ebola
magharibi mwa Afrika inaongezeka kwa kasi mno kwa mamlaka kuweza
kuvidhibiti.
Shirika hilo linasema kuwa zaidi ya watu 2,400 wanadaiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo huku zaidi ya watu 4,800 wakidaiwa kuambukizwa.
Kwa mara nyengine shirika hilo limetoa wito kwa maafisa wa afya kote duniani kuelekea katika eneo hilo ili kutoa usaidizi.
Awali Cuba ilitangaza kuwa inawatuma zaidi ya maafisa 160 wa afya nchini Sierra Leone.
Waziri wa afya nchini Cuba Roberto Morales Ojeda amesema kuwa madaktari wa kwanza na wauguzi watawasili mapema mwezi ujao.
WHO:Visa vya Ebola vimeongezeka kwa kasi
Reviewed by Ino
on
11:32:00 PM
Rating:
No comments:
Post a Comment