WHO kushauri kuhusu dawa ya Ebola

Zaidi ya watu 2000 wamefareiki kutokana na Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi
Shirika la afya duniani linatarajia
kutoa ushauri kuhusu dawa inayoweza kutibu maradhi ya Ebola baadae leo Mjini Geneva kufuatia kikao cha siku mbili cha wataalam wa udhibiti wa magionjwa , watafiti wa tiba, makampuni ya madawa na nchi waathirika .
Hakuna chanjo wala tiba inayofahamika kwa mlipuko wa sasa wa Ebola ambayo ni mbaya zaidi kuwahi kuukumba ulimwengu , ukiwauwa watu wapatao 2000 . Bado visa vya ugonjwa huo vinaripotiwa katika nchi sita za Afrika .
Wataalam 200 wanaokutana mjini Geneva wamekuwa wakichunguza uwezo wa dawa 8 za majaribio ya tiba ya Ebola, na nyingine mbili za chanjo.
Haja ya kubaini aina fulani ya tiba ya ugonjwa huu ni ya dharura. Virusi vya Ebola vinaonekana kuenea kupita kiasi cha uwezo wa kuvidhibiti , huku vifo 400 vinavyotokana na maradhi hayo vikiripotiwa wiki iliyopita pekee.
Mifumo ya afya katika nchi zilizoathiriwa Liberia, Guinea,na Sierra Leone inakaribia kukosa kabisa uwezo wa kutoa huduma za matibabu.
Magonjwa mengine hatari kama Malaria hayataweza kutibiwa . Lakini hata kama mkutano huu utabaini dawa mpya za kukabili maambukizi haya ,hazitakuwa tayari kutumiwa kabla ya mwaka huu.
Wakati huo huo virusi vya Ebola vinaendelea kusambaa , na baadhi ya wanasayansi wanahofu ya kubadilika kwa aina ya virusi hiyo. Mkakati pekee kwa Ebola ni kuudhibiti, lakini juhudi zilizopo kwa sasa hazionekani kufua dafu.
WHO kushauri kuhusu dawa ya Ebola WHO kushauri kuhusu dawa ya Ebola Reviewed by Ino on 10:25:00 AM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.