Meya mwenye utata alazwa hospitalini

Meya Rob Ford amewahi kukiri kutumia dawa za kulevya
Meya wa Toronto, anaekumbwa na utata Rob Ford, amelazwa hospitalini baada
ya kupataikana na uvimbe tumboni mwake.
Alikwenda hospitalini akiwa na maumivu makali ya tumbo. Madaktari hawajaeleza uzito wa tatizo hilo la kiafya la Meya huyo hadi wafanye uchunguzi zaidi.
Bw. Ford, aligonga vyombo vya habari mwaka jana pale alipokiri kutumia mihadarati aina ya cocaine na kuwa anakabiliwa na tatizo la ulevi.
Awali kipindi cha miezi miwili alitafuta usaidizi wa kitabibu kujaribu kuacha uraibu wa kutumia dawa za kulevya na pombe na Alirudi ofisini hapo Juni.
Licha ya hayo amejitosa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mwezi ujao akitafuta muhula mwengine kama meya.
Meya mwenye utata alazwa hospitalini Meya mwenye utata alazwa hospitalini Reviewed by Ino on 2:58:00 AM Rating: 5

No comments:

ino mo. Powered by Blogger.