Mateka mwengine akatwa kichwa na IS
Serikali
ya Uingereza imesema kuwa inachukua hatua za dharura ili kubaini ukweli
wa kanda ya video inayoonyesha mateka wa Uingereza David Haines
aliyetekwa nyara na kundi la himaya ya kiislamu akikatwa kichwa.
Mfanyikazi huyo wa misaada aliyekamatwa nchini Syria mnamo mwezi Machi mwaka jana ameonyeshwa akipiga magoti katika jangwa, kando yake akiwa ni mtu aliyeficha uso wake ambaye amebeba kisu.
Atakuwa mateka wa tatu wa magharibi kukatwa kichwa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
katika kanda hiyo ya Video mtu aliyeshika kisu anaonekana akishtumu mataifa yanayounga mkono Marekani,naye Haines ambaye anaonekana kuwa chini ya shinikizo anaonekana akimlaumu waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron kwa hatma yake.
Mwisho wa kanda hiyo mateka wa pili wa Uingereza anaonyeshwa na kutishiwa.
Wakati huohuo Waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron ameshtumu kukatwa kichwa kwa David Haines kama kitendo cha kishetani.
Amesema kuwa wauaji watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria ata iwapo itachukua mda mrefu.
Katika taarifa yake rais Obama pia ameshtumu mauaji ya kikatili ya David Haines.
Amesema Marekani inaomboleza na Uingereza kifo cha mateka huyo na kungezea kuwa itashirikiana na muungano mkubwa wa kimataifa ili kuwakamata washukiwa mbali na kuharibu tishio hilo kwa ulimwengu.
Wanahabari wawili Steven Sotlof na james Foley waliuawa na wapiganaji hao mwezi uliopita.
Mateka mwengine akatwa kichwa na IS
Reviewed by Ino
on
7:23:00 AM
Rating:
No comments:
Post a Comment